Sababu kubwa kuandika mada hii fupi juu ya ukweli ulokithiri ya baadhi ya wapenzi wasiokuwa na malengo, hivyo ndugu usikubali kabisa mtu akuchezee, tafuta mtu mwenye malengo ujue nini kakusudia juu yako isiwe anataka kusogeza siku tu kisha anakupotezea.

Nimefanya uchunguzi wa kina, nikagundua wapenzi wengi hapa kwetu unguja wanapenda uhusiano wa majaribio, je wewe ni wa majaribio? sasa kwa nini basi unamruhusu mtu aingie kwenye historia yako wakati lengo lake ni kupita tu kwako?

Jamaani inauma sana wakati wa kuachwa mtu ambaye umemkabidhi moyo wako na kumtegemea kwa maisha yako yote ya baadae, kisha anakugeuka na kuhamisha upendo kwa mwengine.

Uwe ndugu Msomaji Zanzibarwebsite siku zote unatakiwa uwe wa kwanza kupigania furaha yako. hawezi kutokea mtu wa pembeni kwenye 4ro chat ambaye akakulaghai kwa maneno matamu kisha baada ya muda akakuondolea furaha yako...kuwa tahadhari.

 

Ndugu msomaji umeubwa na akili hapaswi mtu kukuchezea unatakiwa umsome kabla hujamuingiza moyoni. fungua mlango wako wa huba kwa mtu aliye na uhakika usikubali mwili wako kuwa wa majaribio siku ya siku anakuramba kisogo aibu yako ipo nje wanachama wenzio wanakusema kwa Chemba jinsi maumbile yako yalivyo mwenywe ukiwa hujijui.

Ni mimi Mzee wa nasaha mwanachma mwenzenu.

 

A'malik 

Views: 48

Andika Salamu

Lazima uwe mwanachama wa Zanzibarwebsite ili uweze kuweka ujumbe!

Join Zanzibarwebsite

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service