MAPENZI GANI JUU YA MTUME SAW YANAHITAJIKA ?

Nimeonelea makala yangu hii nianze kwa njia ya maswali juu ya swahiba wa mtume rehema na amani ziwe juu yake.

  Huyu ni Abdullah ibn abu kuhafa (aswiddiq) kama ajulikanavyo alimpenda sana rasulillah saw

>akawa kama bodigadi wakitembea anapinda njia huku nahuku kumzingira habibullah.

>Katajwa katika qurani waziwazi surati A taubah

>Katajwa katika surati Laily na nyinginezo

>Mwanaume bora baada ya mitume na manabii (yaani yeye ndo anawafatia kwa iiman kama wasemavyo wanawazuoni)

> Amali zake ulimwengu wa sasa nadhani kuzifikia ni ndoto.

    Sikwamba maswahaba wengine siwaoni nao pia amali zao si haba nafasi ni ndogo nachelea kukuchosha

    Kina Omar, Uthmaan, Ally na wengineo wote hawa hakuna ibada yoyote ya dini hii ambayo hawakuijua wala hawakuifanya.

   Naachia hapa tuje kwa watu ambao wanajulikana kwa jitihada zao katika dini maimamu wanne wa kutegemewa {abu hanifah, Malik, Ashaffy na Ahmad}jamani walitufunza kuyashughulikia kauli za rasulullah mpaka wakafikia kusema juu ya hofu kwamba madhehebu yao ni hadith za rasullullah saw.

   ???? Napata kizunguzungu wapi unajua???????

                    Yaani hawa wote hawakujua kumsomea mtume saw MAULID ?

                         kama njia ya kumpenda, Kwahiyo sisi wachamungu sana ?

                                   Tunampenda rasulillah saw kuliko hawa waliopita ?

                                                        Tunazijua sana ibada kuliko hawa?

                            maana ushahidi uko wazi hao wote wa juu hawakuyafanya haya.

Wito wangu enyi waislamu wenzangu. Tuache waiga wakristo shubri hadi shubri, na hivi karibuni nimesikia  mwaka mpya wa kiislamu watakiwa kua sikukuu.(ili na sisi tuwe na chrismass(maulid) na mwaka mpya kama wao)

          Wito wangu tusiweweseke mtume wetu saw katupa viwili kama alivyosema katika hadith sahih {zetu ni hizi (ii) kaashiria vidole viwili, kisha kasema idd-elfitri, na idd-udhhaa}.

         Kama mambo yetu tukiyaendesha kwa kufuata mwandamo wa mwezi nanai atataka mwaka mpya kuutangaza wakati kila mwislamu atajua kua kesho ni mwaka mpya.

       

Pia mapenzi gani kwa mambo ambayo hakuyafanya?

Tufunge jumatatu kama kweli tunampenda ili tusherehekee kama yeye hiyo birthday?

Mbona twampenda kwenye wepesi tu ?

           Tujadiliane!!!

Views: 36

Andika Salamu

Lazima uwe mwanachama wa Zanzibarwebsite ili uweze kuweka ujumbe!

Join Zanzibarwebsite

Maoni ya RAUDHA on February 25, 2012 at 3:46pm

Asalamu alaykum musiwe na hitilafu maulid moja kwa moja ni bidaa kwa maelezo mengi kama utataka kufahamu ingia  ALHIDAAYA

Maoni ya maulid idrissa on February 11, 2012 at 11:01pm

Waalaikum salaam warahmatullah wabarakatuh

  > almuhim ndugu yangu muislamu soma historia ya maulid wewe kama wewe !

  > Jiulize huyo Othmani maalim na abubakri ni nani anaempenda mtume ?

  > Hizo fatwa zake namsikia mara nyingi sana zinavuta tu hisia za watu na mahaba na kutafuta umma mkubwa au sapoti, jee tunayoyafanya katika ibada waliyafanya maswahaba wajulikanao ?

   > mimi ntakupa mfano. hivi sasa masheikh wajuzi wa hali ya juu kabisa wanahalalisha riba za simu jee utawafuata kwa sababu ni masheikh na wanajua kuremba lugha na mtiririko mzuri ?

   > Mtume wetu saw alituambia watakuja masheikh wa watu, wa dunia, wa dola na dunia, haya yote yapo ndugu yangu. Achana na masheikh, cha muhim vitabu vipo akwambie ametoa wapi hiyo kisha uende usome acha kulewa na maneno matamu tu,

   > Sisi huku kwetu kuna masheikh wengi sana na wakubwa lakini wanafanya ibada ukimuuliza imeandikwa wapi  anasema tumemkuta babu yetu anafanya lazima tuendeleze.

   Kama haitoshi niambie nikutumie link usome historia ya maulid katika maandishi (hili ndo jina langu usishangae silipendi nimehudhuria maulidini miaka zaidi ya kumi ndipo ikanilazim kufanya  uchunguzi kama walopita welifanya au la)

Maoni ya Issa Suleiman on February 10, 2012 at 7:22pm

Assalam alaykum Ndugu Maulid Idrissa ningependa kukushauri tu ukaingia You tube kisha tafuta othman Maalim Mada kuhusu Maulid ameelezea kwa urefu kuhusu Maulid nadhani baada ya kusikiliza utatosheka kabisa na kama hukutosheka basi no yake ya sim ipo mpigie akufahamishe au kama upo znz ni vizuri ukamfuata akakufahamisha nini Maulid na asili yake. mimi ningelikueleza lakini uwanja ni mdogo hutotosheka nitakuacha na kiu yeye ametumia masaa mawili kufafanua nini maulidi  Ahsante

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service