

KURAAN 2:125.
Na kumbukeni tulipo ifanya ile ALKAABA iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani. Na alipo kuwa akisimama Ibrahim"MAKAAMU IBARAHIIMU" pafanyeni pawe pa kusalia.
Na tuliagana na Ibrahim na Ismail: Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanao inama na kusujudu.

KURAAN 2:126.
Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangui! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini ALLAH na Siku ya Mwisho. Akasema: Na mwenye kukufuru pia nitamstarehesha kidogo, kisha nitamsukumiza kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahala pabaya mno pa kurejea

KURAAN 2:127.
Na kumbukeni
Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ALKAABA wakaomba: Ewe Mola wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.

KURAAN 2:128.
Ewe Mola wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako,
na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

KURAAN 2:129.
Ewe Mola wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Lazima uwe mwanachama wa Zanzibarwebsite ili uweze kuweka ujumbe!
Join Zanzibarwebsite