Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin, protini, wanga na mafuta?.
Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana Mwezi wa Ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu.

Ebu zijue faida zake.
Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee.

Baadhi ya faida zake mwilini ni kama ifuatavyo;

1- Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

3- Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.

4- Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

5- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

6- Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.

7 - Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.

8- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.

9- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.

10- Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.

Views: 233

Kurasa: Afya, Vyakula bora

Andika Salamu

Lazima uwe mwanachama wa Zanzibarwebsite ili uweze kuweka ujumbe!

Join Zanzibarwebsite

Maoni ya salum ali said on August 24, 2011 at 7:29am
Ahsante kwa darsa ya tende.
Maoni ya Ramadhani Msuya on June 18, 2011 at 12:41pm
Nashkru kwa elimu ,Je tende inatatizo kwa watu wenye kisukari endapo watakula
Maoni ya HAJI ATHUMANI TUPPA on June 18, 2011 at 12:00pm
asalam aleykum waungwana matumaini yangu niwazima mie nawapa hai kwani hakika salamu nikama nusu ya kuonana mie nimtanzania mwezenu naomba msinitenge kwani napatikana dar-es-salam maeneo ya mbagala yani kiwanda cha nguo kangha kinaitwa KTM ndipo napatikana mie yangheeeeeeeeee kwa kujitambulisha huko namatumaini ntapata imeli zakufa mtu na mkitaka kuchati na mimi ni hajituppa@yahoo.com na namba ya simu ni 0714-376409 au 0688-994799
Maoni ya Rukky Mwaddy on June 17, 2011 at 11:39am
Nshkuru kwa ilmu niloipata kuhusiana na tende.
Maoni ya Jaffar Shehe - JEFF on April 14, 2011 at 7:25am
asante sana mm nakula sana tende lakini sijui faida zote hizi ulizozitoa,kwani mm hula kwa starehe na kuipenda kwa ule utamu wake,shukran kwa kunielimisha nitazidisha speed ya kula tende kwa kufuata maelekezano yako.
Maoni ya JEWEL on October 4, 2010 at 3:43pm
Tende ni tunda maarufu sana katika nchi za Mashariki ya Kati na sehemu zingine duniani. Umaarufu wake umeanzia maelfu ya miaka iliyopita na pengine ndiyo tunda pekee liliotajwa sana hata katika vitabu vitakatifu vya Mungu.

Wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, matumizi yake huongezeka kwa kiwango kikubwa kwa sababu ya kutumiwa na idadi kubwa ya waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa kufungua swaumu au wakati wa kufuturu.

Lakini pengine ni vizuri kujua siri ya kupendwa na hata kutajwa sana kwenye vitabu vya Mungu kwa tunda hili. Lina umuhimu na faida gani katika mwili wa binadamu kiasi cha kuwa maarufu hivyo?

FAIDA ZA TENDE
Wanasayansi wa masuala ya vyakula wamelishafanyia utafiti tunda hili na kugundua kwamba sifa yake kubwa ni kuwa chanzo kikubwa cha virutubisho na nishati ya mwili (energy). Mtu ukila tende mwili huweza kupata nguvu mara moja.

Hivyo ni wazi kwamba waumini wanaofunga mchana kutwa wanahitaji kula vyakula vya kurejesha virutubisho na nishati mwilini ambayo ilikosekana kwa siku nzima. Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nishati, mtu anaweza kuendelea kuishi kwa kula tende na maji tu.

Tunaelezwa kuwa, tende ina virutibisho muhimu visivyopungua kumi, vikiwemo Calories, Calcium, Protein, Potassium, Magnesium, Phosphorous Vitamin A, Folate, Carbohydrates ambavyo vyote ni muhimu kwa kinga na ustawi wa mwili wa binadamu.

TENDE DAWA YA UKOSEFU WA CHOO
Kwa wale wenye matatizo ya kukosa choo kwa muda mrefu, tende inaweza kuwa suluhisho la tatizo hilo. Imeelezwa na wataalamu kuwa tende ina kiwango kikubwa cha kamba-lishe (fibre) ambazo ni muhimu kwa ulainishaji wa chakula na kuwezesha kupatikana kwa choo kirahisi.

Kama una tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, tumia tende kama dawa ya kulainisha choo (laxative) kwa kuloweka kwenye maji usiku kucha, kisha asubuhi zikoroge katika maji hayo na kunywa juisi yake, fanya hivyo kwa wiki mara mbili.

Aidha, tende imegundulika kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya saratani ya tumbo (colon cancer). Vile vile ina uwezo wa kuimarisha afya ya moyo na kuukinga na maradhi mengine kwa kunywa juisi yake ambayo hutengenezwa kwa kulowekwa kama ilivyoelezwa hapo juu.

Kutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, tende huweza pia kutibu magonjwa mengine ya tumbo, yakiwemo kujaa gesi, kuharisha na kuchafuka kwa tumbo. Kwa wale walevi wa kupindukia, ambao miili yao imejaa sumu, tende huweza kuwa na msaada mkubwa wa kuondoa sumu hizo katika miili yao.

Hivyo basi, tende isiliwe mwezi wa Ramadhani peke yake, bali iwe ni chakula ama tunda la kuliwa wakati wote na watu wote, kwa sababu kila mtu anahitaji kuwa na afya bora, bila kujali imani ya dini aliyonayo.
Maoni ya Badru on October 4, 2010 at 2:30pm
Usijali, hili ni tunda lisilo na mfano kama ilivyo kwa asali, subiri kidogo nitawatumbukizia na maajabu ya asali. Inshallah tuombe uzima.
Maoni ya Al Mabrouk on October 4, 2010 at 12:35pm
Shukuran kwa kutupa faida hii.Hakika matunda ni dawa bora.

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service