Ndugu Zangu.

 

Kwakuwa mimi ni binadamu kama binadamu kama binadamu yoyote yule, udhaifu wangu nimeuona toka mwaka huu kuingia, niweke wazi kwamba mm Abdullmalik Nasser nimepata mke hapa hapa ukumbini udhaifu wangu kwa kwanza ni uchoyo wa kutokualikeni harusi wana ukumbi wenzangu hii nimeifanyia utafiti nikagundua kuwa wivu umechangia kwa hili.

 

kadhalika sitopenda kumtaja mwenza wangu ila katika masharti yetu tulikubaliana kwa ujumla kuwa sote kwa pamoja tusiingie hapa kwenye huu ukumbi japokuwa hapa ndipo pahala tulipojuana....lkn mm nikaenda mbali zaidi  ''siku utakayo ingia hiyo ndio itakuwa TALAKA3 Zako!!  sasa nimefanya utafiti wangu nimegundua kumbe mwenzangu anaingia kwa mlango wa nyuma, (kabadilisha jina) 

 

Suali langu linakuja jee kama mimi (Mume) nimejua na ninaushahidi wa kutosha jee hii itahisabika talaka?

 

Sambamba na hili kubwa zaidi hata nikaandika waraka huu kuwa kwanini inafikia hatua wewe ushajijua ni Mke wa mtu katika sehemu kama hizi nyeti bila kumjua mwezio unae zungumza nae ni nani basi unakurupuka na kutoa number zako za simu na ukijua fika kama wewe ni mke wa mtu!! iwe hapa au facebook  jee huu ndio utandawazi!?

 

Najua kuna wengine watasema nimekuwa muwazi sana  lakini kuna msemi usemo ''Ukweli ndio mama wa uaminifu''

 

A'malik

Views: 103

Andika Salamu

Lazima uwe mwanachama wa Zanzibarwebsite ili uweze kuweka ujumbe!

Join Zanzibarwebsite

Maoni ya Mathna Ahmed on February 14, 2012 at 8:27pm

Baada ya kusoma habari hii nimeona na mimi nitoe mchango kidogo;binafsi yangu naona kama huyu kaka ameamua ''kujoke'' na wanaukumbi lakini kama hili jambo limetokea kweli basi ndo maji yameshamwagika hayazoleki........Bushako umetoa ufafanuzi ya kwamba talaka haikusihi kwa sababu imewekwa katika (''future tense'' nitakuwacha) maneno yako umeyatoa wapi(kuna aya au hadith uliyoitegemea)  nadhani umepitiwa na mameno ya kaka Abdul-Maliki nayacopy paste hapa......

kadhalika sitopenda kumtaja mwenza wangu ila katika masharti yetu tulikubaliana kwa ujumla kuwa sote kwa pamoja tusiingie hapa kwenye huu ukumbi japokuwa hapa ndipo pahala tulipojuana....lkn mm nikaenda mbali zaidi  ''siku utakayo ingia hiyo ndio itakuwa TALAKA3 Zako!!  sasa nimefanya utafiti wangu nimegundua kumbe mwenzangu anaingia kwa mlango wa nyuma, (kabadilisha jina) .....Amesema siku utakayo ingia  hiyo ndio itakuwa Talaka 3 zako kwa hivyo alipoingia aliachika simple as that!talaka hii inaitwa Al Mua-llaq na huyo si mkeo tena na mkiishi  pamoja as husband and wife basi ni kubeba jukumu....(Uliza zaidi kwa wenye elimu ya mambo hayo watakupa ufafanuzi).

Ikiwa wewe kaka ulipaona hapa ni pahala pazuri pa kupata mchumba na hatimaye kuwa mke iweje sasa umkataze kwa masharti magumu kama hayo??? DONT YOU KNOW THAT ''BIRDS OF THE SAME FEATHERS FLOWN TOGETHER''wewe umerudi either kwa kuspy or kwa kuchat na yeye karudi either kwa kukuspy or kuchat na ujue huyo wenzio alifanya mazoea ya kuingia hapa na mazoea ni taabu huyaacha tu mara moja kwa hiyo wewe ulitakiwa umpe ''subsitute'' nyengine ya kufanya , kama ungemuweka busy na things that she likes asingepata mda wa kuingia hapa but ameingia kwa vile amekuwa bored, after all amebadilisha jina kwa vile anarespects her marriage na hakutaka ajulikane kama ni yeye......Suala ya kugawa number ya simu atalijibu yeye mwenyewe alitaka iweje may be hakuwa na nia mbaya lakini desturi za  waume wa waafrika  hupasuka kwa hasira wakijuwa kibaba chengine calls his wife na hapo una haki kaka ya kuwa mad kwa mkeo kutoa number ya simu kwa stranger.

Ushauri wa bure; Vijana tusiingie katika maisha ya  ndoa bila ya kuwa na elimu nayo,hebu tusomeni kwanza,tujue ndoa ni ibada na kama ni hivyo kuna utaratibu wake maalum haijawekwa tu ili tuzaliane na kuwa wengi. Tutizame ni jinsi gani Mtume Muhammad SallaLLAH Alayhi Wasalaam alikuwa akiishi na wake zake,na pia mujuwe kuwa wanawake wametokana na sehemu ya ubavu iliyopinda sana hainyosheki na ukitumia maguvu methods  unaivunja.

Maoni ya ummy on February 13, 2012 at 9:43am

Abdul hiyo talaka inaitwa talaka ya kutundika, talaka ya kutundika ni ambayo mume ameitundika juu ya kitu kingine kuwa kitu hicho akikifanya au akikiacha atakuwa ameachika: mfano mume kusema "ukitoka hapa nyumbani utakuwa umeachika" akitoka atakuwa keshaachika

Maoni ya bushako on February 13, 2012 at 9:04am

KWANZA MALIKI HUJAMBOO, ?

 NIINGIYE MOJA KWA MOJA KIINI CHA SWALI LAKOO,

NITATOWA KIDOGO UFAFANUZI, KWANZA TUELEWE KUWA TALAKA INASWIHI PALE TUU MUME AKITAMKA KUWA NIMEKUWACHA SI MKE WANGU , SIO NITAKUACHA WALA NDIO TALAKA YAKO, ,

UNATAKIWA UTAMKE NIMEKUACHA SIO MKE WANGU, HAPO NDIO TALAKA, VYENGINEVYO BADO HAIJAWA TALAKA KWA MISINGI YA KISSLAMUU  UNATAKIWA UULIZWE TENA HAYO MATAMSHI YAKOO. 

KWA SABABU WW MALIKI UMESEMA ITAKUWA NDIO TALAKA YAKO , UNATAKIWA USEME HIVII,,,,,  UKIINGIYA KWENYE CHAT NIMEKUACHA TALAKA SIO MKE WAN GU , HAPO TALAKA SAHIHI, KWA MISINGI YA KISLAMU, WAISLAMU  KUNA HATUWA TUNAJIFANYIA TUU  BILA YA SHARIA ZA KISLAMU,

LA PILI KUHUSU KUTOIWA NO ZA SIMU , DINI INATUKATAZA KUWA TUZIDHANIANE DHANA MBAYA KILA SIKU, TUNATAKIWA TUDHANIANE DHANA NZURI NDIO MAANA HUKUMU YA KUZINI LAZIMA WAWEPO MASHAHIDI 4  BALEGHE TENA WASHUHUDIE HILO TENDO ,

MALIKI KUTOWA NO ZA SIMU BADO HAIJAWA KOSA ILA KAA NA  MKEO AKUELEZE SAKATA ZIMA PENGINE KATOWA KWA NIA YA KUKOMBA USHAURI KUWA WW UNATONGOZA SANA  WANAWAKE HAPA FORO NA ANATAKA UWACHE HIYO TABIA , PENGINE ANATAFUTA HAKII NA SHARIA ZA KISLAMU ILA TUU HAKUPITA NJIA SAHIHI SASA USIMJADILI KIUBAYA MOJA KWA MOJA MUULIZE KWANZAA'

 TATU TUNAFUNDISHWA KUWA SIKU ZOTEM PENDELEE MWENZAKO LILE UNALOLIPENDA  NDANI YA MOYO WAKO, WW UNAPENDA KUCHAT KISHA MKEO UNAMKATAZA NINI UNAFANYA MALIKI , WW KWA VILE KICHWA UNAMZUNGUKA KISHA  ALIPOFANYA YY UNATAMKA TALAKA HII SIO SAHIHI , KAMA MUNACHAT MUWE NYOTE , KAMA HAMUCHATI MUSICHATI NYOTE , MKUKI KWA NGURUWE TUU MALIKI , JAMANII?

 HAYO NDIO MANENO YANGU MALIKI KAMA UNA ZAIDI UNAJUWA WAPI PA KUNIPATA , 

KARIBU SANA ,

BUSHAKO , BUSHAKIRINA 

Maoni ya Al Mabrouk on February 12, 2012 at 8:37pm

Inategema na madhehebu yako.Kwa mimi ambae sina madhehebu HIYO SI TALAKA.

Maoni ya suley on February 12, 2012 at 12:04pm

Ndugu AbdulMalik,

Neno lako kuwa"siku utakayo ingia hiyo ndio itakuwa TALAKA3 Zako" hii watu wa sheria waita ni talaka iliotundikwa. Na talaka ya kutundikwa ni ile ambayo mume anaiambatanisha kwa kutoke kitu fulani au mke kufanya kitu fulani km ulivyoitundika wewe kwa kuingia humu.

Hukumu yake

Mke akifanya kile ambacho mumewe amekitundikia talaka basi talaka itakuwa imepatika pale atakapo fanya na kwa idadi ya talaka alizo zitaja wakati wa kutundika

 Kwa mujibu huo ndg yangu huyo mke umemuacha talaka tatu km ulivyotaja  wakati watundika talaka yako .

 TANBIIH

 Swala la kutundika talaka si zuri kwani mara nyingi  huwa lina leta majonzi kwa kumuacha mke pasina kupenda na hasa ikiwa mtu katundika kwa idadi ya talaka tatu kwani hawezi kumrejea mpka huyo mke aole na mumewe mingine na wakutane  kimwili kisha amuache kwa ridhaa yake ndo anakuwa hlali kwa mumewe wa kwanza.

 

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service