nimeowa mwanamke , wiki mmoja mm nikapata safafi ya kwenda vietnam kikazi, nikamuacha mke wangu znz yupo kwenye hedhi , narudi baada ya miaka 2 namkuta na watoto 2, nilikuwa namtumia pesa hana shida kwa kweli,  

 1= jeee nimpe talaka  ama nimsamehe ?

2= jeee nikimuacha nidai mahari  yangu?

3= kama nitamsamehe wale watoto itakuwaje? niwatimuwe ama niwahudumie ?

4=kwa kweli nawaombeni ushauri nn nifanye maana nina hasira sana wakati huu.

Views: 92

Jibu Hii

Majibu ya Mjadala huu

Mbona hujafafanua vizuri.Najua kama ulimuoa basi uliingia ndani na jee hujatueleza kama hao watoto ni pacha au laa?

Mwanamke hana makosa wewemsamehee tuu mwenyemakosa nini wewe uliemuacha miaka miwili kutuma pesa sio sababu je kwamahitaji mengine ninani wakumtimizia.Na watoto waende kwa baba yao.

kitanda hakizai haramu

 

 Hutakiwi kumpa talaka  na watoto ulee humjui nani atakae kufaa pia watoto hawana makosa ulitakiwa uondoke na mkeo.kitanda hakizai haramu ni wako hao

Watoto ni wako kwa ndoa ilikamiika kwa maana mara uipomuoa ilipatikana jimai sawa tueleze ho watoto wana umri gani kwa sababu umetuambia uipoondoka yumo kwenye kawaida ya kila mwezi ndugu yangu hicho sio kipimo wengine hutumia mwenzi 2 na huko uchumi unakuwa

Kha!! tena mpe talaka3 bila hata kumuonea huruma!! Mwache yule aliye mtia mimba amuowe, Sasa unatakia nini kulea watoto si wako!!   kumbuka ile methali ya kiswahili '' Mtoto wa haramu hata ukimtia kwenye chupa basi kuna siku atatoa  kidole chake''

A'malik.

Kwa mujibu wa sheria ya kiislamu hao watoto ni wa kwako,kuna Hadithi ya Mtume(S.A.W) isemayo "mtoto  ni wa kitanda" kwa maana kwamba madamu  wamezaliwa ndani ya ndoa basi hao watoto ni wako( hata kama aliyetia mimba ni mwengine).Kuwakataa kua si wako uko utaratibu wa kisheria wa kuwakataa,sio tu kusema hawa si wangu,kuwakataa ni kwa kadhi na suala likifika  kwa Kadhi kinachofuatia ni kitu kinachoitwa Mulaana ,yaani kuapishana na kulaaniana kiutaratibu maalumu,likipita hilo ndoa yenu inakatika automatically na hamuwezi kurudiana tena

nawashukuru walionijibu japo bado sijapata jibu sahihi , kila mmoja anasema na vyake . nikianza kwa   walichangiya =

1= al-mabrouk nimeingiya ndani kwa maana nimefanya naye jimai,a hao watoto sioo pacha wamepishana mwaka moja kila mmoja,

2=kwa mchango wa  haji tupa , bwana haji kazi ni moja ya ibada kukuenda kule kwa sratere ama matembezi ni kwa ajili ya mm na yy mke wangu , hata mtume (s.a.w) alipohajiri makkah alimuacha mkewe kwa lengo maluum , sasa ukisema hana makosa hapo sio sahihi, kwanini yy anizinie? na watoto kuwapeleka kwa baba hilo nitalifanyia kazi,

3= al-forqani kwa hiyo mm si nitakuwa duyuth? na duyuth  dini inasema hataingiya peponi, hapo vipi '

4= ruwaida kwa hiyo hata kama mke wangu ni mzinifu madhali ananisaidia mm nimsamehe tuu, hebu wacha mfumo wako wa kike sema ukweli maana nahitaji mchango wakoo, hata mtoto wa jirani anaweza kunisaidia sio hao tuu kwa hivyo basi , nipe ushauri utakaonifaa bana,

5=bwana mwinyi nilimuacha kwa ushahidi yupo hedhini, na watoto mkubwa na mwka mmoja na miezi 3 na wa pili ni miezi 5,hi wazi kuwa watoto sio wa kwanguu bwana mwinyi , bado nahitaji nasaha zenu jamanii

 nawasubiria maana maamuzi bado sijayafanya ,

Kiislamu watot walizaliwa ndani ya ndoa ni wako .nakuhusu umsamehe au la hilo ni jukumu lako na wala mtu yeyote hawezi kukushauri kwani!inawezekana mw.ke huyo alianza kuzini na hata kama umerudi lakini pia ataendelea kuzini kwa hio hakuna haja ya kumsamehe ,pia upendo kuhusu huyo mke ni ww pekee unaeujua si mwengine kwa hio hilo linabaki kwako kwani sisi hatulioni kama kateleza au kafanya makusudi na ataendelea kufanya ,ndugu yangu siku hizi kuna w.ke wanataka kuolewa kwa kutoa nuksi tuu kama wasemavyo wenyewe kwa hio mw.ke kama huyo hata ufanye nn basi yy haogopi kuachwa kwani shida yake ni kutoa nuksi na yy tayari ushamtoa hio nuksi.

Tujihadhari kusema mambo ambayo hatuna hakika nayo.kwasababu unachokisema hapa anaweza mtu akakitumia na ikawa hoja dhidi yako siku ya kiama.Hakuna jibu zuri kuliko lile utalolitoa katika Kuraan.

 bado naendelea kuwashukuru wajumbe kwa hili, sasa niwaulize kitu jee , kwenye hukumu ya kislam inasema , maana sharia inasema ikithibika kuwa mmoja wenu kazini ndoa haipo , jee kana nikimsaheme si nitakuwa nimo kwenye madhambi mimi?

pili mzinifu hamuowi ila mzinifu mwenziwe au mshirikina, sasa mm kama nikimsamehe si nitakuwa nipo kati ya hao, kusema ukweli mm sijazini hasaa kule vietnam, ila niliowa kule vietnam ndoa ya mkataba, 

hapo jamani munasewmaje ?

 


Quraan 39:53. """""Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya ALLAH. Hakika ALLAH husamehe DHAMBI ZOTE. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."""""

RSS

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service