Mimi ni kijana wa umri wa miaka 27 katika pirika za kimaisha nimepanga mnamo mwaka kesho nianze process za kufunga ndoa lakini suala langu liko hapa .miaka miwili iliyopita babu yangu mzaa baba alinita na kuniambia kama nikitaka kuoa basi naonaje kama nitamuoa mtoto wa shangazi yangu/nilimjibu kama ndoa hizo mara nyingi zinakua na matatizo kwa hio sitaki kujiingiza kwenye matatizo wakati nayajua.akaniambia hakuna matatizo je nimempenda au la?  masuala mengine nimuachie yy .

1=shangazi yangu na mama yangu mzazi hawapatani

2=sina uhakika kama huyo bint mwenyewe kama atakubali au watafanya kumlzimisha

3=mimi mwenyewe nataka nipate mke ambae hatufahamiani kutoka ukoo mwengine ili niweze kuutawanya ukoo

4=mpaka sasa sijui limefikia wapi naogopa kuliulizia na siku ndio zinakwenda .

NAOMBA USHAURI WENU.

Views: 70

Jibu Hii

Majibu ya Mjadala huu

haya ahjsante kwa kuwa muwazi zaidi ndugu yangu bin rajab. lakini

kwanza ufahamu kuna kndoa za aina nyingi karibuni 4 au 4, ndoa ya kislamu, ya kijadi, ya kikabila, na ya kiserikali, 

mm naona tuzungumzie ndoa ya kislam , ndugu yangu mwanamke wa kislamu huolewa na sifa zifuatazo . 

kuwa muislamu, nasab yake , uzuri wake dini yake , na mali yake , sasa hilo lako ww la kuhofia matatizo kwanini useme matatizo , yaani tayari ushalenga negetive , mbona husemi positive za ndoa ya kindugu ?

siku zote ww ndiye unayekwenda kuishi na mwanamke kwa hiyo mtu, mke hachaguliwi ili mukija kukosana ukasemacha  mm wewe sijakupenda kabisaaaa ni fulani tuu ama wazee tuu, walinilazimishaa, sasa  muowe yule uliyempenda hili majuto yasije lujwa mjukuu,

cha msingi hapo kaana wazee wako waeleze mawazo yako  watakuelewa tuu, usiwa kasirikei wala kuwadharau ila sema nao kwa upole watakuelewa tuu, kuwa mm nataka hivi na vilee,  

M/ Mungu' anasema; musiwajibu wazee wenu hata neno dogo la kusema  ... aaaaa, basi unapata dhambi, ukipata baraka za wazee utaweza kuoa mke bora , na wala sio bora mkee,

siku zote woga unampelekea mja kuingiya kwenye uovuu, pambana na haki yako ,kaulize ila tumia lugha nzuri na ya busara kwa wazee , namaliza kwa kukushauri tenaa

mwanammme  mke  hatafutiwi tafuta mwenyewe , mwisho wa ushauri wanguu,



Kaka rajabu nadhani kaka Bushoka kaisha kutajia sifa za mke anaetakiwa kuolewa.Asante sana kaka bushoka kwa kufanya kazi hiyo hakika ni sahihi.

Naweza kuchangia kutoa ushauri kuwa:Mke ni yule uliyempenda wewe si yule aliyempenda mama yako au baba yako,kwa maana kwamba wewe muoaji unayofurasa pana ya kuchagua mwenyewe mke anaekufurahisha sawa sawa awe wa ukoo wako au nje ya ukoo.Kama msicha wa ndani ya ukoo unaona moyo wako wampenda oa kabisa na wala usitizame ugomvi wa kutoelewana wa shangazi yako na mama yako kwani hilo liko nje na masula ya kuoana wawili waliopendana.Na kama unaomuona msicha huyo si kiwango kwa maana huzapendezwa nae basi tafuta yule utakae mpenda maana moyo wako maana ndoo safi ni ile iliyofanyika kwa uhuru zaidi pasina kupelekwa pelekwa na kuchaguliwa.

Hivyo msikilize babu yako lakini pia mwambie feeling zako zikoje,hapo usiingize suala la matatizo hapana maana wewe na binti hamna matatizo cha msingi ni kuangalia unampenda au humpendi,na yeye anakupenda au hakupendi.hilo tu,kama hakupendi au humpendi nenda nje ya ukoo.

Nakutakia mafanikio kibao.

Naam! 

1. waweza kumwambia babu kiungwana kabisa kuwa "JICHO LANGU PALE HALIJATULIYA"

2. waweza piya kumtafutiya huyo binti, mchumba wa kumuowa ikiwezekana hata ukampendekeza BUSHAKO akafanye nusra hapo.

3. Na kama kwa namna moja au nyingine 'unakimezea mate' hicho kitoto cha shangazi, basi itabidi uanzishe mchakato wa kuwapatanisha mamako na shangaziyo.

4. Kisha ukamuulize huyo kimwana kama aweza kupenda kuolewa na mtu sampuli yako

Rajabu wakati ukuta achana na ndoa za ndugu kwa wakti tulionao...

Kauli ya kiungwana ya kumwambia babu chukua hiyo ya Mzee Dikupa......

Ukoo ukiwa una kifafa jua hakiondoki kazi ni kurithishana misiba.

Tafuta atokuridhi Jicho ilokichagua

Moyo utaukabidhi Kulea na kupepea.

Usiifanye ajidhi    Hayo tunokwambia.

Kuoa mbali ni kutanua jiografia yako ili masafa yaongezeke na kujaza watu wakaleta hima wana wakajua wapi pa kukimbilia,isiwe DONGE MBIJI mezaliwa,mesoma hapo ,meoa hapo na kuzaaa hapo ,hebu tanua uwanja uitembee dunia..

HAAAHAHAHAHAHAHA - JUMA KARIM

BIN RAJAB.

Kwanza kabisa nakupa Pole kwa mtihani uliopo mbele yake,

Lakini pia, napenda kukujulisha ya kwamba Majibu yake ni Rahisi mno, kuliko unavyo fikiria.

Mosi, ni vyema ukifahamu ya kwamba Ndoa ni TAASISI,

Taasisi inayoshirikisha watu wawil wa Jinsia Tofauti, yaani Mume na Mke, kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ni budi wawe na Umri wa Kuanzia  Miaka kumi na minane na Kuendelea, Kwa HIARI YAO WAWILI HAO, BILA SHURUTI WALA SHINIKIZO, watamke Mbele ya Kasisi, Kadhi, Sheikh au Mkuu wa Wilaya au afisa yeyote aliye kasimiwa kisheria kufanya hivyo.

Pili Taratibu zote za ki -mila, ni lazima zifutwe, hii ni pamoja na kutuma ombi la uchumba, hatimae kulipa mafungu husika ( mahari ) wapo walipao mifugo, fedha, au zana za kulimia kuwindia n.k.

Mwisho wa Siku, wawili hao, wanaungana na kuwa Kitu Kimoja, yaani Mume na Mke.

wakitekeleza maagizo kadhaa wa kadha, kama itampendeza Mungu, basi nae atawapa ZAWADI ya mtoto au watoto.

Ngoja ni waachie na wenzangu wakushauri nami nitamalizia kipengele cha mwisho kilicho salia.

Pole sana kwa huo mtihani ila kaa ukijua mke mwema unatafuta mwenyewe na si wakutafutiwa na wazazi.

         assalaam alaykum,pole sana Bin Rajab.mimi nitaongezea kidogo tu, umeishaambiwa sifa za mke wa kuoa ni hizo nne,hivyo mwenye sifa kati ya hizo afaa kumuoa, lakini mtume Muhammad swala llahu alayhi wasallam kamalizia kuwa shikama na dini(yaani shikamana na mwenye dini), hivyo bila kujali migogoro iliyopo angalia je huyo binamu yako ana dini? na je! unampenda? maana Allah sub haanah wata'ala ashawambieni oeni katika mnaowapenda,(sunnah na ayah haziachani hivyo ya mtume na ya Allah yanaenda sambamba)

          na pia jiulize je una mwingine unaempenda na ana sifa hizo? ama ushaahidi yeyote kumuoa?

hiyo yote si neno hata kama wangekua kumi, cha msingi zidisha ibada,usibishane na mtu yeyote bali mtake Allah ushauri kwa kuswali sunnat istikhara, naamini kama utaswali kwa yakiyn Allah atakufumbulia fumbo hilo nakukujaalia kufunga ndoa na yule mwema zaidi kati ya wale uwapendao. lakini chunga kwamba Allah ndio akuchagulie na sio wewe tena kama utaamua kuswali sunna hii.kwa upana zaidi na maelekezo ya swala hii ingia www.alhidaaya.com    utaikuta huko.nakutakia kila la kheri na Allah akufanyie wepesi inshallah.Amiiiiiiiiiiiin.

Nashkuru sana wadau wote kwa ushauri wenu hasa wale waliojaribu kutumia mifano na maandiko kutoka katika kitabu kitukufu cha qur an .vile vile ningependa kuwataarifu kama sio wote baadhi yao tayari wao naufanyia kazi na inshallah utanisaidia ninaiman na vile vile napenda kuwashukuru pamoja na kunishauri lakini pia walijaribu kuingiza mzaha ili mistari ichangamke kidogona  kunichekesha na wanaofatilia mada hii.

NB: huu mchakato naendelea nao lakini pia nitajitahidi kila hatua nitakayo piga nitajaribu kufahamisha wadau zaidi ili kama panahitajika ushauri basi munisaidie kabla sijakosea na kujilaumu. AMIIN

RSS

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service