naanza kwa bashasha,  maneno  yangu kutoka

nimeijaza  bahashaaa,   pomoni  hadi  kufika

dhamira yangu tamasha, mchumba kwenda mposa.





mahari nimeshaweka ,     hilo  kwangu halina shaka

begi  nimeshaliwekaa,     nyumba rangi nishapakaa

mke jamani namtakaa,    kiudhati hasa natamkaa

natafuta mshenga akifika, ruhusa kwao naitafuta.







mshengaaa   ukifika ,       ujumbe wangu fikishaa

mwera njia ya chwaka,   nyumbani kwa baba aisha

siku saa dakika ikifikaa,   muda mzuri baada ya isha

usijivishe  makabokaa,    mshenga nanakufundishaa.







mahari  kidogo upatane,   dunia imeharibikaa

isifikie  hata  laki  nanee,   tuwasiliane kukuharibika

mtoto mwari siye mjane,   hakuvimba kama pakaa

wanasema namba nane,    mshenga usijebabaishwa.







mshenga  ukienda lazimisha,   ifanyike  akdi haraka

watu  wote nitahamasishaaa,   inshallah kharusi itafika

jimai bushako  nitakamilishaa, hehehe nitazaa kama paka

mshenga tena nakuharakisha,  wengine waweza nipita.





ni bushako, bushakire, bushakirina,



















Views: 8

Jibu Hii

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service