MAKOMBO !!
Kila alae makombo Hujiona kafaidi
Wewe ulie mrembo Hili usilikaidi
Walionasa urimbo Wanalijua zaidi
HUJIONA KAFAIDI KILA ALAE MAKOMBO
Tembea ufike ng'ambo Tena uweke juhudi
Useme chako kimombo Sudi umwite Juedi
Kujitanda kwa mapambo Makombo uyafaidi
KILA ALAE MAKOMBO HUJIONA KAFAIDI
Yana nini majigambo Asazae kafaidi
Huna lako tena jambo Wa awali kakuzidi
Nimeyafumbua mambo Wazi iwe makusudi
HUJIONA KAFAIDI KILA ALAE MAKOMBO
Kata mti iwe fimbo Tengeneza mjeledi
Yake thamani makombo Chake cha shibe uledi
Nahodha kwakwe ni chombo Makombo kuwa baidi
KILA ALAE MAKOMBO HUJIONA KAFAIDI
Hitimisho langu jambo Na ukome ufisadi
Mambo yaendao kombo Yameingia kuadi
Leo nishaimba wimbo Kiitikio menadi
HUJIONA KAFAIDI KILA ALAE MAKOMBO
Kurasa:
Permalink Imejibiwa na bushako on February 14, 2012 at 3:18pm hehe, hehe, hehe, hehe. haha , haha, haha, haha.
ni na cheka kwa dhihaka. babengwa limekufika.
wewe panya mimi paka. moyo wako umevurugika.
ongoza njia uking'aka. makombo wenzio twayataka.
nakuhisi una jambo. ila kulisema hutaki.
kuyaponda makombo . hakuna ila umehamaki.
wapi yako majingambo. mtoto ninaye kiembe samaki.
siyajali yako mafumbo. nitakualika siku yakula keki.
makombo huwa makombo. ikiyashiba na vinywaji.
lakini hili la mwanakombo. umelikosa kwa ujuajii.
ulijifanya wewe ni mbogo. kutembezwa kwa vibajaji.
umekuja na wako ungooo. utawezaje kuyaweka maji ?
kwangu wala si makombo. walitambuwa kwa hakika.
naijiiibu yako hii tungo. waweza uka kasirikaaa.
huyu binti ana maungoo. umehumiwa bila shakaa.
bushako ala hana maringo. babengwa utaishia kubweka.
bushako bushakirina...
Permalink Imejibiwa na Dikupa on February 19, 2012 at 3:22am mla hasa mla leo, mla jana kala nini,
fakhariye simulio, yungali njaa tumboni,
mla na maendeleo,leo ana kitu gani,
kala nini mla jana,
mla hasa mla leo!
haja mkidhi sihaba,hatokoti maungoni,
mla leo akashiba, fakhariye shukurani,
wajana wake msiba, hana leo mkononi,
kala nini mla jana,
mla hasa mla leo!
huyajutiya makombo, kayasaza kulikoni,
aloyapiga kikumbo,kwa isirafu mezani,
leo bakuli na chombo, atafuta muhisani,
kala nini mla jana,
mla hasa mla leo!
anatetema baridi, joto halipo mwilini,
anatamani yarudi, makombo kwenye sahani,
kama jana kafaidi, leo karaha, huzuni,
Kala nini mla jana,
mla hasa mla leo!
nakaditama Dikupa, tano siyo khamsini,
ila si vyema kutupa, ingali ina thamani,
japo kipande mfupa, kina mchuzi jikoni,
kala nini mla jana,
mla hasa mla leo!
Dikupa Dikupatile dikilema (cheko lenye afya)
Permalink Imejibiwa na Abdullmalik on February 22, 2012 at 9:32am Wacheka nini mchekwa , Bushako umepagawa
Babegwa alokwitika . hakuna wa kukutuwa
nyamaza sije tapika, Makombo yakakuuwa
Babegwa hasara yako, thamani umejitoa
unachekwa na wenzako, makombo ulovamia
chagua chaguo lako, umeondoka na chua
Babegwa utabakia, kuchekwa na kuzomewa
Kipitacho kurukia, Mwisho watakuondowa
Bushako achekelea, yupo kwake amepowa
Babegwa hutahayari? huna lako lilikuwa
Wanifanya nighairi, kuandika yangu nia
kanuni huzikariri, Makombo wayavamia
A'malik
Shirika la kiswahili Halina zake inadi
Shida ikikukabili Kwao kicheko huzidi
Hukupetea kabali Fedhuli hutaradadi
POLE KWAO HAWAJALI
Kama hili hukubali Tizama hao wawili
Fadhila hata kwa hali Waniwekea kufuli
Nani ataekubali Shirika la kiswahili ?
KWAO POTELEA MBALI..
Makombo ukiwa huli Hilo lina afadhali
Nimekoma ufedhuli Nyie msioniojali
Zipunguzeni shughuli Wa moja havai mbili
CHEI CHEI YENU !!
Permalink Imejibiwa na Abdullmalik on February 25, 2012 at 11:00am Wakiambiwa ukweli, hujifanya kuhamaki
Wasingizia kiswahili, Batili iwe ya haki
tulia nikupe ukweli, sipate taabu na dhiki.
Hasira mwisho hasara, Faraha mwanzo hilaki
Usijitie papara, Mkali huambiliki
Uamuzi wa hasira, Wewe mtu si samaki.
Kwangu mimi ni furaha, Mkizi ukihamaki
Huona nyota ya jaha, Navua bila mikiki
Wacha nile zangu raha, Nimeekewa na keki.
Bebegwaa ......Punguza Jazba hahahahahaha
© 2012 Created by zanzibarwebsite.com.