washauri     nauliza , akili yanizunguka

usewaza   nimeuliza, jawabu sijalipata

nimepita pia  bakiza,  pamoja na bakita

cheupe cheusi kwanza,bushako vinanitanza.



viwili    nimefishika ,  mikononi  ninavyo

kuna watu wavitaka, kwenda navyo bagamoyo

njia panda  nimefika, nauuumiza wangu moyo

nambieni  kwa  hakika, ninavyo shaurimoyoo.



cheusi chanipendeza,  na cheupe kadhalika

kuviacha   sitaweza ,    maini   yanikatika

napigwa kama pweza, kijasho kinanitoka

mwenzenu nikwenye kizaa, mwanga wenu wahitajika.



bushako bushakirina

Views: 17

Jibu Hii

© 2012   Created by zanzibarwebsite.com.

Lebo  |  Report an Issue  |  Terms of Service